Msaada
Vigezo vya Mfanyakazi Hodari & Sifa za Wagombea
Vigezo vya Kumpata Mfanyakazi Hodari
Katika Ngazi ya Kurugenzi, Kitengo na Kanda
Mahusiano Kazini
Working Relationships
Uwezo wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wengine, kuishi vizuri na wafanyakazi wenzake pamoja na kujenga heshima kutoka kwao.
Umakini na Usahihi
Accuracy
Uwezo wa kutekeleza kazi alizopangiwa kwa usahihi bila makosa.
Uzingatiwaji wa Muda
Timeliness
Uwezo wa kukamilisha kazi alizopangiwa kwa wakati kulingana na ratiba iliyopangwa.
Ufanisi
Efficiency
Uwezo wa kutumia rasilimali zilizopo kwa ufanisi ili kufikia matokeo yaliyokusudiwa.
Ubunifu
Innovativeness
Uwezo wa kuanzisha mawazo mapya kwa ajili ya kuboresha utendaji wa Taasisi.
MUHIMU: Utekelezaji wa kazi kulingana na vigezo vilivyokubaliwa wakati wa tathmini ya utendaji kati ya msimamizi na mtumishi — ikiwa ni pamoja na matokeo na maendeleo ya utendaji kazi kupitia mfumo wa PEPMIS (si chini ya 60% ya maendeleo ya utendaji).
Sifa za Jumla kwa Wagombea
General Eligibility Requirements
(i) Awe hana rekodi ya utovu wa kinidhamu katika mwaka husika unaozingatiwa.
(ii) Endapo ni mtumishi mwenye mkataba wa kazi kwa kipindi maalum, ni lazima awe ametumikia mkataba huo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja (1).
(iii) Endapo ni mtumishi aliyehamia COPRA kutoka taasisi nyingine ya Serikali, ni lazima awe amehudumu COPRA kwa kipindi kisichopungua miezi sita (6).
(iv) Kama ni mtumishi wa FULL TIME ni lazima awe amethibitishwa kazini.
(v) Awe ametekeleza majukumu yake kikamilifu, kwa ufanisi na kwa ufanisi wa hali ya juu kama ilivyokubaliwa katika PEPMIS.